Good news ninayotaka kukusogezea nii kutoka Tanesco ambapo Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene September 18 2015 aliongea mbele ya Waandishi wa habari kuhusu mradi wa bomba la gesi na kuwashwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Ubungo na Kinyerezi.
Maneno yake yalikua haya >>> ‘Mtakumbuka kwamba mwezi mmoja hivi uliopita nilikutana nanyi kuwapa taarifa juu ya maendeleo ya mradi wa bomba la gesi na mitambo ya kuzalisha umeme kwa gesi pamoja na majaribio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika mifumo hiyo‘ – George Simbachawene
‘Mtakumbuka kwamba mwaka 2012 serikali ilianza mchakato wa kutekeleza mradi mkubwa wa bomba la gesi ambalo kukamilika kwake kungesaidia sana kuondoa matatizo ya umeme nchini.Kazi hiyo ilijumuisha ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi wa madimba (Madimba Processing Plant), mtambo wa kuchakata Gesi wa Songosongo (SongoSongo Processing Plant) na Bomba kubwa la kusafirisha gesi kutoka Mtwara na kuja Dar es Salaam‘ – George Simbachawene
‘Hata hivyo mitambo iliyoanza kuzalisha umeme ni ya Megawati 90 tu kwa sasa. Tunaendelea kufuatilia ufanisi wa bomba na hasa msukumo wa gesi pamoja na vigezo vingine vya kitaalamu kabla hatujawasha mitambo mingine.Hii ni kwasababu mfumo wote wa bomba ni mpya na tunapoigiza mitambo hii inabidi tuiingize kwa uangalifu kuepusha madhara katika mfumo wa bomba’ – George Simbachawene
‘Sambamba na hilo,, kila mtambo una kiwango chake cha msukumo wa Gesi kinachoruhusu mtambo husika kuwaka, hivyo kwa kadri viwango vya msukumo wa Gesi katika Bomba vinavyozidi kuimarika ndivyo uzalishaji wa umeme utakavyoendelea kuongezeka.Hii ina maana kwamba upungufu wa umeme uliokuwepo utaendelea kupungua hatua kwa hatua kulingana na mitambo hii inavyoendelea kuwashwa na kuzalisha umeme’ – George Simbachawene
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.