Club ya Yanga SC leo ilikuwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa kwanza wa round ya awali ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya Makundi ya CAF Champions League.
Yanga SC walikuwa wenyeji wa Township Rollers ya Botswana na katika mchezo huo wakiwa nyumbani wamejikuta wakiambulia sare dakika za majeruhi baada ya kusawazisha kupitia kwa Patrick Sibomana dakika ya 86 kwa mkwaju wa penati baada ya awali dakika ya 30 kukosa penati.
Township Rollers wao walipata goli mapema tu dakika ya 7 kupitia kwa Phenyo Serameng, Yanga watahitaji kwenda Botswana mchezo wa marudiano wakicheza mchezo wa kushambulia.
Yanga hawana kumbukumbu nzuri dhidi ya Township Rollers kwani msimu wa 2017/2018 alipoteza hapa kwa magoli 2-1 na alipokwenda Gaborone Botswana alitoka sare 0-0 na kuondolewa kwa aggregate ya 2-1, hivyo sasa hivi atabidi kwenda na mbinu mbadala kuhakikisha anaondoka na matokeo chanya.