Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo amezindua mpango wa nishati endelevu kwa wote (SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030 ambapo amesema uwekezaji wa umeme vijijini awamu ya tatu utagharimu zaidi ya Trilioni moja.
>>>“Mpango huu umelenga kukamilika mwaka 2030 lakini sisi Tanzania kabla ya mwaka huo tutakuwa na umeme kwa kila mtanzania na programu hii italifanya taifa letu lijulikane duniani kwani tuna dhamira ya kumfanya kila mtu apate umeme”
“utasaidia suala la ajira na kutokomeza umaskini, kwahiyo kama nchi tuko katika ngazi za juu za huu mradi katika kuufanikisha tukishirikiana na wadau mbalimbali” – Profesa Muhongo
‘Programu hii ya umoja wa mataifa itasaidia sana katika kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwani inafanana sana na ile ya kwetu ya Taifa ambapo tutazalisha umeme mwingi kutokana na gesi, makaa ya mawe, umeme wa maporomoko ya maji, umeme wa Jua, joto ardhi na mabaki ya mimea’
Mashirika mengi yamesaidia katika kufanikisha upatikanaji wa umeme vijijini ikiwemo benki ya Dunia ambayo imetoa dola milioni 200, umoja wa ulaya umetoa Euro milioni 180, nchi za Nordic zimetoa dola milioni 300 pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika nayo imetoa fedha.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
ULIKOSA HII TAARIFA ZA KUGUNDULIKA KWA GESI MPYA TANZANIA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI