Umoja wa Mataifa unasema kuwa wafanyakazi 88 kutoka shirika lake la kuhudumia wakimbizi la Palestina UNRWA wameripotiwa kuuawa tangu kuanza kwa mapigano tarehe 7 Oktoba.
Idadi hiyo inawakilisha “idadi kubwa zaidi ya vifo vya Umoja wa Mataifa kuwahi kurekodiwa katika mzozo mmoja,” kulingana na taarifa ya pamoja kutoka kwa wakuu wa mashirika yote makubwa ya Umoja wa Mataifa.
Taarifa hiyo inaeleza kukerwa na idadi ya vifo vya raia huko Gaza na kutoa wito wa “kusitishwa mara moja kwa mapigano ya kibinadamu,” huku pia ikitaka Hamas iwaachilie mateka waliowateka nyara kutoka Israel.
“Siku 30 zimepita. Imetosha. Hili lazima likome sasa,” ilisema taarifa hiyo.