Umoja wa Mataifa Jumanne umetoa tahadhari kuhusu mapigano yanayoendelea karibu na eneo lililokuwa salama la Wad Madani nchini Sudan ambapo idadi ya watu iliongezeka na kufikia zaidi ya 700,000.
Vikosi vya akiba RSF, Jumapili viliweka kambi karibu na Wad Madani, ambapo mashambulizi yao yamesababisha maelfu ya watu kuukimbia mji wa pili wa Sudan na kituo cha zamani cha misaada, wengi wao wakiwa tayari wameyahama makazi yao.
Wanajeshi hao wameendelea kusonga mbele zaidi ndani ya jiji, mashuhuda wanasema. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ana wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za mapigano kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na vikosi vya akiba katika eneo la Wad Madani, katika jimbo la Al-Jazira,” msemaji wake Stephane Dujarric amesema.
Tangu mapigano yaanze Aprili 15 mji wa Wad Madani, uliopo kilomita 180 kusini mwa Khartoum, umekuwa kimbilio la maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wakati wa mzozo.