Umoja wa Ulaya umesema utautafakari uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kupiga marufuku safari kati ya Marekani na nchi za umoja huo, kama sehemu ya mkakati wa Serikali yake kupambana na virusi vya corona.
Marufuku hiyo ambayo haihusishi Uingereza ambayo siyo tena mwanachama wa Umoja wa Ulaya, itadumu kwa siku thelathini na itaanza kutekelezwa kuanzia usiku wa kesho Ijumaa.
Kupitia mtandao wa Twitter, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel amesema chochote kinachoweza kuvuruga uchumi kinapaswa kuepukwa na kwamba Umoja wa Ulaya unafanya kila juhudi kuzuia kuenea kwa homa ya virusi vya corona, ijulikanayo kama COVID-19, sambamba na kufanya juhudi kubwa katika utafiti juu ya kirusi hicho.
Marufuku ya usafiri iliyotangazwa na Rais Trump itawahusu watu wote wasio raia wala wakazi wa Marekani, lakini Ikulu ya Marekani, White House imesema haihusishi bidhaa.
KAKA YAKE MSIGWA AFUNGUKA UHUSIANO WAO “MAGUFULI KWETU NI KAYEMBA”