Umoja wa Wakandarasi umesema kuwa unatarajia kutoa helikopta kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yenye thamani ya Bilioni 10 na kiasi cha milioni 100 kununua mafuta kwaajili ya usafiri huo utakaosaidia katika shughuli za kampeni za uchanguzi mkuu.
Wakizungumza jijini Dar es salaam wamesema kuwa hatua hiyo ni katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia katika ujenzi wa miundombinu ambayo imewasaidia kupata fursa za kufanya kazi zao za ujenzi wa miundombinu.