Wahudumu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Jumatatu wameonya kuhusu hali mbaya kwenye hospitali za kaskazini mwa Gaza huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa operesheni za ardhini za jeshi la Israel.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imesema hospitali za Shifa na Al Quds katika mji wa Gaza na hospitali ya Indonesia kaskazini mwa Gaza, zimeshambuliwa mwishoni mwa juma.
Shirika hilo limeongeza kuu hujuma hizo ziliifuatia wito uliotolewa upya na jeshi la katili la Israel la wagonjwa kuondoka katika vituo hivyo vya afya mara moja.
Kwa mujibu wa OCHA, takriban watu 117,000 waliokimbia makazi yao wanahifadhiwa katika hospitali 10 ambazo bado zinafanya kazi katika mji wa Gaza na mahali pengine kaskazini mwa Gaza, ambazo zimepokea maagizo ya kurejewa kwa wito wa kuondoka katika siku za hivi karibuni.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kupitia ukurasa wake a X lnalo imesema “kuhamishwa kwa hospitali nzima haiwezekani bila kuhatarisha maisha ya wagonjwa”.