Umoja wa Mataifa umesema wiki hii kwamba wanawake wamekuwa na wakati mgumu wa kupata fursa za kazi ulimwenguni kuliko ilivyodhani hapo awali.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterress ameeleza hayo na kuongeza kuwa mwanya wa jinsia katika hali makazini na malipo haujabadilika sana katika kipindi cha miongo miwili, wakati dunia ikisherehekea siku ya kimataifa ya wanawake.
“Usawa wa jinsia unazidi kuwa na mwanya mkubwa Kwa mwenendo wa sasa, idara ya UN Women inauweka uko mbali kwa miaka 300” katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema kwenye hotuba yake kabla ya siku ya kimataifa ya wanawake leo Machi 8, wakati alipokuwa akizindua majadiliano ya wiki mbili yanayoongozwa na tume ya hadhi ya wanawake.
“Matokeo ya janga la Covid 19 yanaendelea kwa mamilioni ya wasichana waliolazimika kuacha shule, kina mama na watoa huduma wamelazimika kuacha kazi za kulipwa ,watoto wametumbukizwa katika ndoa za mapema”.
Kuanzia Ukraine mpaka Sahel, mizozo na migogoro inawaathiri wanawakena wasichana kwa kiwango kibaya sana na katika kiwango cha kimataifa, baadhi ya nchi hivi sasa zinapinga kujumuishwa kwa dhana ya jinsia katika mashauriano mbali mbali,” amesema Guterres.
Kwa mujibu wa data mpya za ILO, asilimia 15 ya wanawake walio na umri wa kufanya kazi duniani wangependa kuwa kazini, lakini hawana ajira, ukilinganisha na asilimia kumi na nusu ya wanaume.
Mwanya huu wa jinsia bado haujabadilika kwa miongo miwili, ilisema taarifa.
Shirika hilo la kazi la Umoja wa Mataifa limegundua kwamba mwanya wa kajira ulikuwamkubwa sana katika nchi zenye kipato cha chini, ambako karibu robo ya wanawake wanashindwa kupata kazi.
Guterres ametaka hatua za pamoja kote duniani zichukulie na serikali, jamii za kiraia na sekta binafsi kutoa elimu inayojibu masuala ya jinsia, kuboresha mafunzo ya ujuzi na kuwekeza zaidi katika kuziba mgawanyiko wa jinsia kidigitali.