Katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres ameeleza wasiwasi wake kuhusu kukamatwa kwa waangalizi wa uchaguzi nchini Zimbabwe wakati huu pia kukiwa na madai ya kutishwa na kuhangaishwa kwa kupiga kura.
Kiongozi huyo wa UN kupitia msemaji wake, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa nchini humo na wafuasi wako kuepukana na njia zozote za uchochezi na kwamba kuna haja ya kuheshimiwa kwa haki za binadamu na sheria ya taifa hilo.
Tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza rais Emmerson Mnangagwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata asilimia 52.6 ya kura zote zilizopigwa.
Licha ya tangazo hilo la tume ya uchaguzi, upinzani kwa upande wake unasema ulishinda katika uchaguzi huo, ukisema kulikuwepo na udaganyifu.Waanaglizi wa uchaguzi wamesema zoezi hilo halikuafikia vigezo wa kidemokrasia.
Wiki iliyopita, zaidi ya waangalizi 40 walikamatwa wakijaribu kuainisha matokeo yao na yale ya tume ya uchaguzi.