Ustaa wa David Beckham si tu kwenye soka..baada ya kustaafu soka amekua akishiriki katika mambo mbalimbali ikiwemo mitindo pamoja na kushiriki shughuli za kijamii.
Jana Shirika linalosimamia haki za watoto UNICEF limemzawadia tuzo ya heshima staa huyo baada ya kuonyesha mchango mkubwa katika kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Sherehe za yuzo hizo zilifanyika jana huko Beverly Hills na kuhudhurikiwa na baadhi ya mastaa akiwemo Mariah Carey ambaye alikua akitoa burudani, Selena Gomez, Lionel Richie, Elton John, Michelle Rodriguez, pamoja na Nicole Kidman.
Beckham alifanikiwa kupata tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kushiriki kwenye shughuliza jamii ikiwemo kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kupitia miradi yao.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.