Leo June 18,2018 tunayo story kutokea Mahakamani Kisutu ambapo imeambiwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kudondoka ghafla alfajiri.
Hayo yameelezwa na wakili wa Mbowe, Jeremiah Mtobesya mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, wakati kesi ya viongozi wa CHADEMA ikiendelea.
Tunaye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya CHADEMA, Tumaini Makene ambapo amezungumzia hali ya Mbowe.