Uongozi wa Klabu ya Simba umesema Muharami Said Mohammed maarufu Shilton hakuwa Muajiriwa wa Simba SC.
“Simba ilimuomba na kukubaliana na Muharami kuwanoa Makipa wetu kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo Klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa Magolikipa, kwa mantiki hiyo Klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo”
“Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa Klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo”
Itakumbukwa mapema leo Mamlaka ya dawa za kulevya imewataja Watuhumiwa tisa (09) waliokamatwa kwa kukutwa na Heroin akiwemo aliyetajwa na taarifa hiyo kuwa ni Kocha wa Makipa Simba SC. ambaye pia ni Mchezaji wa zamani wa Simba Muharami Said Mohamedi (40).