Wakati uchaguzi wa serikali za mitaa ukitarajiwa kufanyika harakati mbalimbali zimeongezeka maradufu, na ni wazi sasa kwamba ushawishi wa mitandao ya kijamii katika uchaguzi huo utakuwa mkubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Athari za mitandao ya kijamii kama nyenzo ya kuwasiliana kisiasa tayari zimeanza kuonekana kufuatia ukuaji wa mitandao hiyo kama Vile Twitter, Facebook, WhatsApp, Instagram na YouTube.
Wataalam wanasema kuwa ushawishi unaotolewa na mitandao ya kijamii katika siasa unatokana na uwezo wa mitandao hiyo kuharakisha mawasiliano na kuwafikia wapiga kura bila ya kutumia vyombo vya habari.
Huku idadi kubwa ya wapiga kura wakiwa vijana wanaotumia sana teknolojia ya kidijitali ikiwemo simu aina ya smartphones na mtandao, wagombea watakao kuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi huo ujao watakuwa wale wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii.
Ni muhimu wa kufahamu kuwa upo umuhimu wakati huu kutumia mitandao kwa faida katika uhuru wa kujieleza ili kutovunja sheria kwa kutoa taarifa za uongo kupoteza umma wakati huu muhimu.
Lakini pia ni muhimu kutambua kuwa ili kujilinda dhidi ya kuenea kwa taarifa za uongo, ni muhimu kuendelea na ukuzaji wa taarifa sahihi kuhusu masuala muhimu ktofanya hivyo kunaweza kupelekea kwa kuzimwa au kukwamishwa kwa ufikiaji wa mitandao muhimu itakayokuwezesha kupata taarifa muhimu kwenye sehemu tofauti tofauti au hata juu ya chaguzi mbalimbali.
Utafiti unaonyesha kuwa kuzimwa kwa mitandao kunaathiri makumi ya mamilioni ya watu duniani kote kwa namna mbalimbali na serikali ndio huwa inatoa agizo la kuzimwa kwa mitandao ili kuhakikisha kuwa kuna usalama na kuzuia kwa taarifa ghushi iwapo kuna taafifa za upotoshaji au zinazo weza kuathiri nchi au jamii fulani.
Serikali imeendelea kutoa elimu ya Mpiga Kura ambayo hutolewa kwa wananchi wote kwa lengo la kuwawezesha kuelewa kuhusu Sheria, Kanuni, Taratibu za mchakato mzima wa Uchaguzi, wajibu wao na umuhimu wa kushiriki katika Uchaguzi.