Vikosi vya Zimamoto na Uokoaji Afrika Kusini vimesema vimefanikiwa kuudhibiti moto mkubwa ambao ulizuka katika Bunge la Afrika Kusini mjini Cape Town mapema leo na kusababisha moshi mkubwa huku jengo zima likikabiliwa na hatari ya kuteketea.
Moto huo unaaminika kuanza katika moja ya majengo ya zamani katika eneo la Bunge na kusababisha kufungwa kwa eneo hilo lililoko karibu na Kanisa ambapo Askofu Mkuu Desmond Tutu alizikwa jana kwasababu za usalama.
Msemaji wa idara ya huduma za dharura mjini humo amesema paa lilishika moto pamoja na jengo la Bunge na kusema moto huo umethibitiwa na majengo hayo kuripotiwa kuwa na mianya.
Hakuna ripoti za majeruhi na chanzo cha moto huo pia hakijabainsishwa.