Katika Msimu wa sikukuu za Christmass na Mwaka mpya madereva 21 wamefutiwa leseni zao huku 24 wakiwa wamepelekwa Mahakamani na zaidi 1090 wamepigwa faini za papo hapo na 3000 wameonywa
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ramadhani Ng’azi akiwa katika Stendi ya Magufuli katika ukaguzi uliofanya na Polisi pamoja na Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA.
Kamanda Ng’azi “Makosa tuliyowakamata nayo Mwendokasi kutoimiza abiria kufunga mikanda, kupita magari ya mbele bila tahadhari, nidhamu imeongeza sana kwa Madereva kipindi cha mwisho wa mwaka, kama tulivyomalizia Mwaka basi tuanze mwaka salama”
Pia Polisi na LATRA wameanza ukaguzi wa magari Shule ambapo Kamanda amesema mbali na ubovu hayatakiwi kuwa TV, Redio
“Bodaboda wasisafirishe Watoto chini ya miaka tisa, magari ya Shule yenye TV zing’olewa tukizikuta tutawashtaki, tumegundua baadhi yao wanapiga miziki na kuonyesha video zisizo na maadili” Kamanda Ng’azi
Nae Mkurugenzi wa LATRA CPA Habibu Suluo amesema “Wanafunzi wameanza kwenda Shule Mikoani hivyo LATRA wameweka kambi kwenye Stendi ili kuhakikisha usafiri unapatikana.
“Wanafunzi wengi leo wanarudi shuleni kunawezekana kukawa na uchache wa mabasi tupo hapa kutoa vibali vya dharula, jana tumetoa vibali mabasi matano yaondoke kwa dharula kwenye njia ambazo sio za leseni zao” CPA Habibu Suluo