Kufuatia Mvua ilionyesha April 23 mjini Geita iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha kuezua paa za Kaya 42, mapema April 25 Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amefika eneo la Katumaini Mzingamo mtaa wa Nyamalembo kata ya Mtakuja kusikiliza na kutoa pole kwa Wananchi waliobomokewa nyumba zao huku akitoa elfu 50 kwa kila Kaya kwa familia 9 zilizoathirika na mvua hiyo ikiwa ni sehemu ya kujikimu kwa chakula kwa kipindi hiki.