Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kufuatia vurugu za mashabiki wa Urusi zilizotokea katika mchezo wa Euro 2016 kati ya England dhidi ya timu ya taifa ya Urusi, limekaa na kuanza kujadili namna ya kuidhabu Urusi kutokana na vitendo hivyo.
UEFA inaijadili Urusi kutokana na mashabiki wake kuwafanyia fujo, kuwapiga na kuwafanyia vitendo vya kibaguzi mashabiki wa timu ya taifa ya England katika mchezo uliochezwa jana June 11 2016 katika mji wa Marseille na kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Kwa mujibu wa shuhuda anaeleza vurugu hizo zilizoendelea hadi nje ya uwanja, zilianzia ndani ya uwanja wakati ambao mechi ilikuwa ikikaribia kumalizika baada ya shabiki wa Urusi kurusha miale ya moto kwa mashabiki wa England, kufutia tukio hilo UEFA inatarajiwa kutoa adhabu kali kwa Urusi.
ALL GOALS: TAIFA STARS VS MISRI JUNE 4 2016, FULL TIME 0-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE