Urusi imezindua chanjo ya Saratani inayotumia teknolojia ya mRNA ambayo ni tofauti na chanjo nyingine za kawaida, Chanjo hiyo inakusudia kusaidia mwili wa binadamu kutambua na kupambana na seli za Saratani kwa usahihi na inatarajiwa kuwa na manufaa makubwa katika matibabu ya Saratani duniani.
Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Tiba ya Mionzi, Andrey Kaprin amesema majaribio ya awali yanaonyesha kuwa chanjo hiyo inaweza kuzuia ukuaji wa uvimbe na kuzuia Saratani kusambaa katika sehemu nyingine za mwili hivyo inaweza kuwa silaha muhimu ya kuutokomeza ugonjwa huo.
Inaelezwa kuwa chanjo hiyo mpya inafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya mRNA ambayo inaelekeza seli za mwili kutambua na kushambulia seli za Saratani, Hatua hiyo ni kubwa katika mapambano dhidi ya Saratani, kwani inatoa njia mpya ya kumaliza ugonjwa huo kwa njia ya kisayansi.
Chanjo hiyo inatarajiwa kutolewa bure kwa Wagonjwa kuanzia mwaka 2025 ili kufanya matibabu ya Saratani kupatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu, Serikali ya Urusi inajivunia kutoa chanjo hiyo bure kwa lengo la kusaidia Wagonjwa wa Saratani haraka iwezekanavyo hasa wale wenye uhitaji.