Urusi inakabiliwa na changamoto za kusambaza risasi na silaha kwa wanajeshi wake waliopo katika vita nchini Ukraine, kulingana na maafisa wa Magharibi.
Inakabiliwa na “changamoto kubwa” katika kupata vifaa vya kutosha na nyenzo, afisa mmoja amesema.
Madaia hayo yanakuja wakati wasiwasi juu ya utoaji wa silaha za Magharibi kwa Ukraine unaongezeka.
Wakati vita vinaingia mwaka wake wa tatu, usambazaji wa risasi, silaha na wanajeshi unaonekana kuwa jambo muhimu.
“Uwezo wa uzalishaji wa risasi za ndani za Urusi kwa sasa hautoshi kukidhi mahitaji ya mzozo wa Ukraine,” afisa wa Magharibi alidai, akisema Moscow imeweza kuongeza usambazaji wake tu kupitia kutafuta vyanzo mbadala vya risasi na silaha, ambavyo sio vya muda mrefu. – suluhisho la muda.
Walitaja athari za vikwazo kama sababu moja.
“Vikwazo vinaathiri pakubwa viwanda vya kijeshi vya Urusi, na kusababisha ucheleweshaji mkubwa na gharama zinazoongezeka. Kutokuwa na uwezo wa kufikia vifaa vya Magharibi kunadhoofisha sana uzalishaji wa Urusi wa mifumo mipya ya silaha na rekebishaji wa mifumo ya zamani, huku kukiwa na athari kubwa katika siku zijazo kutokana na ubora wa silaha inazozalisha,” walisema.
Urusi imepiga hatua hivi majuzi, kama vile kuutwaa mji wa Avdiivka, na inaonekana kuwa na uwezo wa juu kwenye uwanja wa vita.