Rais wa Urusi Vladimir Putin aliuambia mkutano wa kilele na viongozi wa Afrika mjini St Petersburg siku ya Alhamisi kwamba Urusi inaweza kuchukua nafasi ya mauzo ya nafaka ya Ukraine barani Afrika, na kwamba Moscow itakuwa tayari kuanza kusambaza nafaka za bure kwa nchi sita “katika miezi ijayo”.
Nchini Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky alitembelea mji wa kusini-mashariki wa Dnipro ambako alijadili kuhusu vifaa vya kufyatua risasi kwa wanajeshi na ulinzi wa anga. Soma blogi yetu ya moja kwa moja kwa maendeleo yote ya hivi punde. Nyakati zote ni za Paris
Wiki iliyopita, Moscow ilikataa kuongeza muda wa mkataba huo ambao ulikuwa unatoa nafasi kwa nchi ya Ukraine kusafirisha nafaka yake kupitia kwenye bahari nyeusi kwenda masoko ya kimataifa ikiwemo Afrika.
Nchi ambazo zitanufaika na mpango huo wa Urusi ni pamoja na Burkina Faso, Zimbabwe, Mali, Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Eritrea.
Putin amesema nchi yake imepanga kuzipa nchi hizo kati ya tani 25,000 hadi tani elfu 50,000 za nafaka.