Katikati ya uvamizi wake nchini Ukraine, Urusi inatangaza silaha zake za hivi punde katika maonyesho ya kijeshi nje ya Moscow.
Wizara ya ulinzi inasema kandarasi za serikali zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 55 zimetiwa saini katika Jukwaa la Jeshi 2024.
Inasema haya ni pamoja na usambazaji wa mifumo ya kisasa ya virusha moto, mizinga, helikopta, makombora ya kuongozwa, na boti za kuzuia hujuma.
Wizara hiyo inasema jeshi litapokea zaidi ya aina 500 za silaha na zaidi ya vitengo milioni 1 vya silaha.
“Wazo la jumla la biashara yetu ni uundaji wa silaha ambazo zitakuwa bora kuliko analogi zilizoagizwa nje na kuturuhusu kuwa na faida kwenye uwanja wa vita,” anasema Vitaly Bulgakov, naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kijeshi.
Shirika la habari la Urusi, TASS, linasema takriban wajumbe 110 rasmi wa kijeshi na makampuni ya kigeni wanahudhuria kongamano hilo.
Inakuja wakati vikosi vya Ukraine vinasema kuwa vinasonga mbele zaidi ndani ya Urusi, baada ya kuvuka mpaka katika eneo la Kursk zaidi ya wiki moja iliyopita.