Urusi itachukulia ndege za kivita za Magharibi za F-16 zinazotumwa Ukraine kama tishio la “nyuklia” kwa sababu ya uwezo wake wa kubeba silaha za atomiki, Waziri wa mambo ya nje nchini humo Sergei Lavrov amesema.
Kyiv imekuwa ikitoa wito kwa washirika wake nchi za Magharibi kuipa ndege za kivita za kisasa haswa wakati huu inapopambana dhidi ya mashambulio ya Urusi.
Lavrov amezungumzia kuhusu mpango wa Marekani wa kuipa Kyiv ndege za kivita aina ya F-16, ingawa Washington haijatoa idhini kwa nchi yoyote kuzisambaza.
“Urusi haiwezi kupuuza uwezo wa ndege hizi kubeba silaha za nyuklia. Hakuna uhakikisho wowote utasaidia hapa,” Lavrov alinukuliwa akisema na wizara ya mambo ya nje ya Urusi.
Uholanzi na Denmark zinaongoza mpango wa kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kuhusu kutumia ndege hiyo iliyotengenezwa nchini Marekani kama sehemu ya muungano wa mataifa 11.
F-16 ni ndege yenye majukumu mengi na inaweza kusanidiwa kubeba silaha za kinyuklia za mbinu.
Vikosi vya anga vyaAmerika ,Ubelgiji na Uholanzi vina F-16s na ujumbe huo, mataifa mawili ya mwisho yakiwa na jukumu la kubeba silaha za nyuklia kutoka kwa ghala la Amerika huko Uropa, kulingana na Bulletin of the Atomic Scientists. Lakini F-16 zozote ambazo zinaweza kuhamishiwa Ukraine hazitakuwa na uwezo wa nyuklia, Hans Kristensen, mkurugenzi wa Mradi wa Taarifa za Nyuklia katika Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani, aliiambia Business Insider mwezi uliopita.