Shirikisho la Soka Duniani ( FIFA ) jana lilijibu shinikizo la kimataifa linaloongezeka kuhusiana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine likisema Urusi itacheza mechi zake za nyumbani katika viwanja visivyoegemea upande wowote na vilevile haitoruhusiwa kuimba wimbo wa Taifa na au kupeperusha bendera za Urusi kwenye mechi.
FIFA imesema kwenye taarifa yake kwamba itaendeleza majadiliano na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na Mashirika mengine ya michezo ili kuangazia hatua yoyote zaidi ama vikwazo ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutengwa kwenye michuano hiyo iwapo hali haitaimarika haraka.
Tangazo hilo linatolewa wakati mataifa hayo mawili yakiwa yamefuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia mwakani huku Ufaransa na Uingereza, Sweden Jamhuri ya Watu wa Czech zikisema hazitocheza na Urusi.