Mazingira machafu ni miongoni mwa changamoto zinazokabili nchi nyingi duniani ambapo ongezeko la watu,sehemu za biashara na kukua kwa miji zimetajwa kama sababu kubwa inayochangia mazingira machafu hasa sehemu za mijini.
Leo April 24 2017 nimekutana na hii list ya nchi 10 zinazotajwa kuwa na mazingira masafi licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, list hii ni kwa mujibu wa Environmental Performance Index .
1:Switzerland
Switzerland ni miongoni mwa nchi zenye mazingira masafi duniani ambapo wameweza kupambana na mazingira machafu kwa zaidi ya asilimia 87.67 ,kwa mujibu wa Environmental Performance Index Switzerland ni miongoni mwa nchi zenye hewa safi.
2:Luxembourg
Environmental Performance imeipa Luxembourg asilimia 83.29 na kuifanya kuwa nchi ya pili kwa mwaka 2017 kuwa na mazingira masafi duniani.
3:Australia
Australia imeshika namba tatu kwa nchi zenye mazingira masafi kwa mwaka 2017 na kwa mujibu wa Environmental Performance index Australia imeweza kupambana na mazingira machafu kwa asilimia 82.4.
4:Singapore
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zinazotajwa kama kitovu cha biashara duniani Singapore pia ni moja kati ya nchi yenye mazingira masafi ambapo imeweza kupamba na uchafu kwa zaidi ya asilimia 81.78.
5:Czech Republic
Czech Republic imeshika namba tano kati ya nchi zenye mazingira safi kwa mwaka 2017 kwa mujibu wa ripoti ya Environmental Performance index .
6: Germany
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi inazotembelewa kwa wingi lakini hii haifanyi ujerumani kuwa nchi chafu,kwani mwaka 2017 imeweza kushika nafasi ya sita miongoni mwa nchi safi zaidi duniani.
7:Spain
Kwa mujibu wa Environmental Performance Index Spain imeshika namba saba kati ya nchi zenye mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na uchafu kwa zaidi ya asilimia 79.79
8:Austria
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zenye amani duniani Austria inatajwa pia kuwa moja ya nchi yenye mazingira safi na imeshika nafasi ya 8 kwa mwaka 2017.
9:Sweden
Sweden inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na uchafu kwa zaidi ya asilimia 78.9
10:Norway
Norway ni nchi ya kumi kwa kuwa na mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na mazingira machafu kwa zaidi ya asilimia 78.04
VIDEO:Ulimiss hii interview ya Ridhwani kikwete akimuongelea Manji?Bonyeza play kutazama.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo