Unadhani mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt bado ana ndoto za kuvunja rekodi kwa kutumia sekunde 20 kwenye mbio za mita 200? jana alikua katika mashindano mengine yakiwa ni ya kwanza tangu mwaka huu uanze.
Mwanariadha huyo jana alishiriki katika mashindano ya Golden Spike yaliyofanyika katika mji wa Ostrava huko Jamhuri ya Czech na aliweza kushinda katika shindano lake la kwanza kwa mwaka huu japokuwa ameshindwa kuvunja rekodi yake ya kutumia sekunde 20, kwenye mbio za mita 200.
Katika shindano hilo lililofanyika jana Bolt alitumia sekunde 20.13 ikiwa ya rekodi yake ya dunia ya sekunde 19.19 baada ya kumshinda Mmarekani Isiah Young.
Kwa sasa Bolt anajiandaa kwa mashindano ya dunia yatakayofanyika Beijing mwezi August mwaka huu.
Naye Asafa Powell ameshinda katika mbio za mita 100 akitumia sekunde 10.04.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.