Hali ya ulinzi na Usalama wa wandishi wa habari mkoa wa manyara Imezidi kuimarika Baada ya Jeshi la Polisi Na waandishi wa Habari kufanya midahalo mbalimbali ya Kugundua Changamoto zinazowakabili wandishi wa habari na kuzitatua.
Hayo Yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha wandishi Wa Habari Mkoa waManyara Zacharia Mtigandi wakati wa Mdahalo wa kujadili ulinzi na usalama wa waandishi wa habari ambapo amesema hakuna madhila yaliyofanyilwa kwa waandishi wa habari Kwanzia mwezi january mwaka huu hadi mwezi machi ndani ya mkoa huo.
Kwa Upande mwingine Mwenyekiti wa kamisheni ya uchunguzi Wa kisayansi mkoa wa manyara SSP MAGAI TUMAINI CHASSA amesema wandishi wa habari wanatakiwa kuwa waadilifu kuwa na nidhamu nà kuzingatia maadili ya kiuandishi.
Wandishi wa Habari waliodhuria katika mdahalo huo wamema kuimarika kwaulinzi na usalama wao Itazidi kuwapa motisha Ya Kufanya kazi Nzuri yenye mànufaa katika jamii.