Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam(DAWASA) @dawasatz Mhandisi Mkama Bwire amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kinondoni kufikia asilimia 97%.
Akizungumza katika Kikao Kazi cha DAWASA na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Wilaya ya Kinondoni, Mhandisi Bwire amesema “Tuchukue nafasi hii kumshukuru Mheshimwa Rais kwa kinondoni kazi ya maji imefanyika na bado kazi inaendelea kufanyika”
Mhandisi Bwire ameeleza kuwa asilimia hizo 97% ni zile ambazo serikali imefikisha mtandao wa mabomba ikiwa inaendelea na kazi ya kuwavutia wateja wao maji.
“Kinondoni ina kata 20 mitaa 126 tumefika kwenye mitaa yote lakini kazi inaendelea. Serikali imefanya kazi yake ya kupeleka mtandao wa mabomba kwa 97% kuna kazi ya pili ya kuhakikisha ambapo sasa mtandao umefika watu wanajiunganisha kwenye mtandao huo”
Mhandisi Bwire ameeleza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na Wenyeviti wa mitaa ili kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na huduma ya maji safi na salama.