Ulimwengu kwa sasa umeshuhudia ukuaji mkubwa wa matumizi ya teknolojia na pia intaneti lakini watumiaji wengi wa teknolojia hizi wamekua katika hatari ya kuingia katika matumizi mabaya ya teknolojia hii kutoka na wizi na vitendo vya udhalilishaji vinavyoweza kutokea kupitia mitandao.
Wanaharakati mbalimbali wamejitokeza wakifundisha na kuhimiza matumizi salama ya mitandao hii kwa namna mbalimbali. Mfano, tunahimizwa kulinda akaunti zenye za mitandao ya kijamii kwa nywila (Password) imara na kutoziweka wazi kwa watu wengine
Unashauriwa kufikiria vyema kabla ya kufanya jambo lolote ikiwemo kutoa maoni, kutuma picha, video au kutumia maneno fulani ili yasije yakatumika vibaya dhidi yako na yakaathiri shughuli zako.
Wapo watu ambao walikosa kazi, walipoteza heshima zao na nafasi zao kutokana na mambo waliyoyatuma kwenye mtandao miaka ya nyuma na wakasahau ila mitandao iliweka taarifa na kumbukumbu ya matukio yao.
Hivyo, huu ni ukumbusha na wito kuwa mimi na wewe tuwe makini na chochote tunachotuma au kuchangia katika mitandao ya kijamii ili kufanya ushiriki wetu uwe salama kwetu na kwa watumiaji wengine.