Makubaliano ya kusitisha mapigano, yametiwa saini na wawakilishi wa jeshi na wale wa wapiganaji wa RSF, baada ya mazungumzo ya mjini Jeddah na sasa yataanza kutekelezwa rasmi kuanzia siku ya Jumatatu.
Chini ya makubaliano haya, mbali na usitishwaji wa mapigano, pande hizo mbili zitatakiwa kutuhusu kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu kwa raia walionaswa kwenye mapigano.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema, haifahamiki ikiwa mkuu wa majeshi ya Sudan jenerali Abdel Fattah al Burhani na mwenzake anayeoongoza kundi la RSF Mohamed Dagalo, watakuwa tayari kuheshimu makubaliano ya safari hii.
Wawakilishi wa jeshi la Sudan, wakiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, wamekubaliana kusitisha mapigano kwa wiki moja, kuanzia Jumatatu, Marekani na Saudi Arabia zilitangaza katika taarifa ya pamoja siku ya Jumamosi.
Pande hizo hasimu za kijeshi zimekuwa zikisisitiza kuendelea na vita, kila mmoja akidai kuwa lengo lake ni kuibuka mshindi katika vita ya kuwania madaraka yanyoendelea na ambapo imeingia wiki ya 6.
Tangu kufanyike mapinduzi ya kijeshi, Sudan imekumbwa na mzozo mkubwa, maandamano ya kila wiki, ukandamizaji mbaya ambao uliua zaidi ya watu 100, na uchumi wake kuzidi kudorora.
Huku mazungumzo hayo yakifanyika katika mji mkuu Khartoum, mamia ya watu walikusanyika mashariki mwa mji huo wakiomba utawala wa kiraia, katika maandamano ya hivi karibuni dhidi ya mapinduzi ya tarehe 25 Oktoba yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan.