Usitishwaji wa mapigano kati ya Israel na Hamas umeorefushwa kwa siku mbili katika Ukanda wa Gaza, Qatar imetangaza Jumatatu hii, Novemba 27. Hamas imethibitisha habari hiyo. Makubaliano haya yalipaswa kumalizika alfajiri siku ya Jumanne, kulingana na makubaliano ya kwanza; hapa usitishwaji mapigano umerefushwa saa 48, yaani hadi Alhamisi, Novemba 30 asubuhi.
Usitishwaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza, ulioanza Ijumaa Novemba 24 saa 5:00 alfajiri saa za Mashariki ya Kati , unmerefushwa kwa siku mbili.
Uamuzi huo umetolewa Jumatatu hii, Novemba 27. Usitishwaji wa mapigano unapaswa kudumu kwa siku sita na kwa hivyo utaendelee hadi siku ya Alhamisi, Novemba 30 saa 7:00 aubuhi saa za Mashariki ya Kati.
mateka waIsrael na wafungwa wa Kipalestina wanatarajiwa kuachiliwa huru Jumatatu hii, kwa mujibu wa makubaliano kati ya Israel na Hamas wataachiliwa usiku.
Mateka wa Hamas wanapaswa kuachiliwa, sawa na wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa katika jela za Israel. Kwa mujibu wa Gazeti la Le Parisien, watoto watatu, raai wa Ufaransa wanaweza kuachiliwa huru na kundi la Hamas.
Tangu Jumamosi, misafara mirefu ya misaada ya kimataifa inaendelea kuingia katika Ukanda wa Gaza kutoka Misri.