Raia wa Mali wanatazamiwa kupiga kura siku ya Jumapili kutoa uamuzi kuhusu katiba ya serikali ya nchi hiyo, ambayo imechochea uvumi kuwa mtawala shupavu wa nchi hiyo atawania kuchaguliwa.
Kura hiyo ni ya kwanza kuandaliwa na jeshi tangu iliponyakua mamlaka mnamo Agosti 2020 katika nchi iliyokumbwa na mzozo wa kisiasa, usalama na kiuchumi kwa miaka mingi..
Lakini chini ya miezi tisa kabla ya tarehe ya mwisho, Mali haina ufafanuzi juu ya jukumu la baadaye la jeshi, akiwemo kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita.
Wananchi wa Mali watapigia kura rasimu ya katiba kuanzia saa 0800 GMT siku ya Jumapili, kukiwa na kura za kijani kwa kura ya “ndio” na nyekundu kwa “hapana” na matokeo yanatarajiwa ndani ya masaa 72.
Mamlaka zimewekeza sanakatika mageuzi hayo huku makundi ya kijihadi yakiendelea kufanya mashambulizi ya umwagaji damu kwa raia na wanajeshi
Inakusudia kurekebisha katiba ya sasa ya nchi, iliyopitishwa mwaka 1992 na mara nyingi kulaumiwa kwa matatizo ya Mali.
Na iwapo itaidhinishwa, katiba mpya itaimarisha nafasi ya jeshi, ikisisitiza “sovereignty”, maneno ya junta tangu kuingia madarakani na baadae kuachana na ukoloni wa zamani Ufaransa.