Ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na wananchi kunufaika na rasilimali za madini, Serikali kupitia Tume ya Madini ilifanya maboresho mbalimbali ya Sheria ya Madini na kanuni zake yenye lengo la kuhakikisha kunakuwepo na ongezeko la ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini na Serikali kupata kodi mbalimbali sambamba na kuzalisha ajira zaidi.
Moja ya maboresho ni pamoja na kutungwa kwa kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content) ambazo zimeleta manufaa kwa wadau wa madini hususan wananchi wanaoishi jirani na migodi ya madini.
Tume ya Madini ina jukumu la kusimamia ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ili kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa zilizopo katika Sekta ya Madini pamoja na kufungamanisha Sekta ya madini na Sekta nyingine za kiuchumi.
Akielezea uanzishwaji wa kanuni hizo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba hivi karibuni kupitia mahojiano maalum alieleza kuwa lengo la kuanzishwa kwake lilikuwa ni kuongeza ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini kuanzia kwenye shughuli za utafutaji wa madini, uchimbaji wa madini, masoko ya madini sambamba na kutoa huduma kwenye migodi ya madini kama vile ajira, ulinzi na vyakula.
Aliendelea kusema kuwa lengo lingine lilikuwa ni kuhakikisha kampuni za uchimbaji wa madini zinatumia bidhaa zinazozalishwa nchini badala ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi hivyo kuwezesha wananchi kujipatia kipato huku Serikali ikipata kodi mbalimbali.
Akielezea manufaa yaliyopatikana tangu kuanzishwa na utekelezaji wa kanuni husika, Mhandisi Samamba alisema kuwa mpaka sasa asilimia 86 ya kampuni za wazawa zinatoa huduma na bidhaa migodini