Ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambapo Mei 9, 2024 amewasilisha Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2024/25 Bungeni mkoani Dodoma.
Hizi ni nukuu zake alichozungumza Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti hiyo.
‘Pia Utekelezaji wa mradi wa kuboresha mfumo wa Usambazaji maji katika jiji la Mwanza unaogharimu Shilingi Bilioni 4.62 umefika asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kunufaisha Wakazi wapatao 33,000.Aidha Utekelezaji wa mradi wa kuboresha mfumo wa usambazaji maji eneo la Ilemela unaogharimu Shilingi Milioni 405.64 umefikia asilimia 70 na unatarajia kukamilika mwezi Juni 2024 na kunufaisha wakati 12,000’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Vile utekelezaji wa mradi wa kupanua mtandao wa usambazaji maji katika miji ya Magu na Misungwi unaogharimu Shilingi Bilioni 1.94 unaendelea hadi mwezi April 2024 utekelezaji umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa imekamilika utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Chujio la Butimba kwa gharama ya Euro Milioni 31.17 sawa na takribani Shilingi Bilioni 80.19 kukamilika kwa mradi huo, kumeboresha huduma ya maji kwa wakazi wapatao 450,000 katika jiji la Mwanza’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Wizara imekamilisha utekelezaji wa mradi wa majisafi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 233.9. Kukamilika kwa mradi huo kumeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita Milioni 40 hadi Milioni 200 kwa siku na hivyo kukidhi mahitaji ya maji kwa Jiji la Arusha, kuongeza huduma ya uondoaji wa majitaka kutoka asilimia 7.6 hadi 30%, na kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 48 hadi 39’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso