Mtaalamu wa ugharamiaji wa huduma za afya wa mradi wa HPSS tuimarishe afya unaotekelezwa hapa nchini na Taasisi ya Swiss Tropical and Public Health kwa ufadhili wa Serikali ya Uswisi, James Kidumba amesema utoaji huduma za afya kidigitali umekuwa njia sahihi ya kuleta mapinduzi ya mifumo ya afya kulingana na utaratibu mzuri wa utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambako kulikuwa kukifanyikka Mkutano wa 10 wa Kongamano la AfyaTanzania Health Summit).
Akizungumza na waandishi wa habari Kidunda ameeleza kwa kina kuhusu taasisi yao ambavyo imekuwa ikitekeleza mradi wa Health Promotion and Syestem Strengthening (HPSS) chini ya ufadhili wa Serikali ya Uswiz.
Ameongeza kwamba ndani ya Kongamano hilo la nne la mkutano wa 10 umewakutanisha na wadau mbalimbali pamoja na watalaam wa masuala ya afya sambamba kuwasilisha jumbe zao ambazo zinabebwa na dhana ya tafiti.
Amesema wao kama wadau mwaka huu tafiti zao zimejikita katika uboreshaji wa mfumo wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ,katika vituo vya kutolea huduma kupitia mfumo wa ushitindi ambao unahusika uchangiaji au upunguzaji wa nafasi iliyokuwa imeachwa katika upatikanaji wa dawa na Bohari ya Dawa (MSD).
Ameongeza kupitia mkutano huo wametoa mapendekezo yao yakiwemo kuongeza uboreshaji zaidi ya mfumo hasa katika upande wa utoaji wa huduma kidigitali katika upatikanaji wa dawa.
Amefafanua kumekuwa na mapinduzi makubwa katika upande wa utoaji wa huduma ya afya kiteknojia kwa miaka mitano kutoka sasa kurudi nyuma.
“Mifumo ya kidigitali ikiendelea kuimarisha katika utoaji wa huduma za afya itasaidia kurahisisha uwasilishaji wa taarifa na kuwafikia viongozi katika ngazi tofauti tofauti za maamuzi kwa urahisi na kuweza kuzifanyia kazi.”
Wakati huo huo Mwakilishi na Mratibu wa Bima ya Afya ya Jamii( CHF) Mkoa wa Dar es Salaam Walter Amandusi amesema kupitia Ibara ya 83 (i) katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM imeelekeza wananchi wengi wapate huduma za afya kupitia bima.
Ambapo amesema Serikali iliamua kutengeneza bima za afya kwa wananchi ambao hawapo katika mfumo rasmi ambao unaitwa CHF ambapo 2022 uliboreshwa na kuitwa ICHF.