Mifuko ya uwekezaji wa pamoja unaosimamiwa na UTT amis wamneanzisha kampeni ya uwekezaji kwa jamii yenye lengo la kuwafikia watu wengi zaidi kuwekeza katika mifuko hiyo ya kampeni iliopewa jina la kijiwe mchongo na UTT amis.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam jana , 25-7-2024 Mkurugenzi wa masoko na mawasiliano wa UTT Amis Bw.Daudi Mbaga amesema, lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwafikia watu wote popote walipo kupitia majukwaa tofaut tofauti kama vile youtube,insta na vile vile hata kwenye maredio na vyombo mbali mbali vya habari ili iweze kuwafikia wanufaika haraka zaidi.
Aliongeza kuwa kufwatia uzinduzi wa program hiyo itakayoitwa Kijiwe Mchongo na UTT Amis watanzania hilo ndo litakuwa jukwaa lao huru amablo wanaweza kujifunza masuala ya uwekezaji na pia njia rahisi kwa watanzania kushiriki katika uwekezaji ulio salama na wenye historia nzuri katika mitaji na dhamana.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa uendeshaji wa UTT Amis, Bw Issa Wachichinenda ameomba wananchi mbali mbali wachangamikie fursa kwasababu ukiwekeza na UTT ni kwamba umewekeza sehem salama na ni uhakika kupata pesa yako mda wowote utakaohitaji.