Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru mwanafunzi wa kike kulipwa fidia ya KSh 4 milioni sawa na Tsh. milioni 87 baada ya picha zake akiwa nusu uchi kutumwa kwenye mitandao ya kijamii na polisi.
Inaelezwa kuwa tukio hili lilitokea August 2015 baada ya msichana huyu aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari Kanyama kukutwa na misokoto ya miwili midogo ya bangi ambayo alikuwa ameificha kwenye nguo yake ya ndani.
Hata hivyo inaelezwa Mahakama ilifikia uamuzi huo wa kuamuru fidia ilipwe kwa kuwa polisi waliingia matatizoni baada ya kutuma picha kwenye mitandao wakiwa wanamsachhi mwanafunzi huyo huku akiwa nusu uchi jambo lililotafsiriwa kuwa la udhalilishaji.
HEKAHEKA: Mwanamke aliyepokonywa mtoto wa miezi 10 mpaka leo ana miaka mitatu