Leo December 15, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imewaachia kwa dhamana wanawake waliokamatwa baada ya video yao ya kuvalishana pete ya uchumba kusambaa kwenye mtandao ya kijamii.
Dhamana hiyo imepatikana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini bondi ya Tsh Milion 6 kwa kila mmoja ambapo jumla ya watuhumiwa wa tukio hilo ni wanne.
Wanne hao ni pamoja na Milembe Suleiman, anayedaiwa kumvalisha pete mwanamke mwenzake Janeth Shonza, pamoja na watuhumiwa wengine wawili ambao ni Richard Fabian aliyerekodi video hiyo na kuisabaza pamoja na Aneth Mkuki aliyekuwa akiongoza sherehe hiyo yaani MC.
FULL STORY: Wanawake waliovishana pete Mwanza Mahakamani