Marufuku hiyo inajiri baada ya afisa wa mawasiliano wa Uturuki kukosoa jukwaa hilo kwa kile alichosema ni uamuzi wa kuzuia machapisho ya rambirambi kwa mauaji ya mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh mapema wiki hii.
Mtandao maarufu wa kijamii wa Instagram umezuiwa nchini Uturuki, Mamlaka ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya nchi hiyo (BTK) ilisema Ijumaa, bila kutoa sababu yoyote kwa nini au kidokezo cha muda gani marufuku hiyo itawekwa.
Ufikiaji wa programu ya simu ya mkononi ya Instagram pia umezuiwa.
Tovuti ya BTK inasema: “Instagram.com imezuiwa na uamuzi wa Mamlaka ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya tarehe 02/08/2024 na nambari 490.05.01.2024.-608983.”
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun kuikosoa Instagram kwa madai ya kuzuia machapisho ya rambirambi kwa kifo cha Ismail Haniyeh – mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas ambaye aliuawa katika shambulizi la alfajiri huko Tehran, Iran siku ya Jumatano.