Uturuki imeadhimisha miaka 101 ya kuanzishwa kwa Jamhuri yake huku kukiwa na sherehe nchi nzima zinazoadhimisha siku hiyo ya kihistoria.
Shughuli zimeanza kwa sherehe mjini Ankara, ambapo Rais Recep Tayyip Erdogan, pamoja na viongozi wa serikali na jeshi, walitoa heshima zao Anitkabir, katika kaburi la mwanzilishi wa jamhuri Mustafa Kemal Ataturk.
Erdogan amehimiza ukakamavu na ari ya Uturuki katika kuendeleza fikra za Ataturk za maendeleo ya kisasa.
Sherehe hizo zimefanyika nchini kote, huku kukiwa na shughuli za aina yake Istanbul, pamoja na maonyesho ya kuvutia katika eneo la Bosphorus.
Wananchi, kuanzia watoto mpaka viongozi, walikusanyika kushuhudia magwaride, matamasha na fataki, wakionyesha umoja na fahari. Kimataifa, balozi za Uturuki zimehodhi shughuli kama hizo, zikionyesha umuhimu wa uwepo wa Uturuki duniani.
Maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Jamhuri hayakuenzi tu safari ya kihistoria ya Uturuki, lakini pia yameonyesha mafanikio ya Uturuki na malengo yake, hasa katika nyanja za kiuchumi na maendeleo ya kijamii.