Siku mbili baada ya Chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ kutangaza mikakati mitatu ya kupinga ilichokiita ukandamizaji wa haki na demokrasia na kuitangaza siku ya September mosi mwaka kuwa ni siku ya maandamano nchi nzima.
Leo July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi wa Manyoni Singida na kutoa onyo kwa watakaoanzisha maandamano, Rais Magufuli amesema…..
>>>’Wasije wakanijaribu mimi ni tofauti sana, na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa, siasa nzuri wananchi wetu washibe, wapate madawa, nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni’
https://www.youtube.com/watch?v=oYNX71a-DGc
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUSEMA KUWA HAWAKUINGIA KWA SABABU WALIJUA NAO NI PART YA HAO MAFISADI, UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI