Ijumaa ya December 15 2017 historia mpya imeandikwa katika Ligi Kuu England kupitia staa wa kimataifa wa Misri anayecheza soka la kulipwa katika club ya Liverpool Mohamed Salah ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Misri kuwahi kushinda tuzo EPL.
Mohamed Salah ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia kutokea Misri kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu England msimu 2017/2018, wapo wachezaji wa Misri kama Amr Zaki waliowahi kucheza England lakini hakuna aliyewahi kutwaa tuzo hiyo.
Leo December 15 Mohamed Salah ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi November wa Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 akiwa na takwimu za kucheza game nne kwa mwezi November na kufanikiwa kufunga magoli saba ndani ya mwezi November.
UTANI: Haji Manara kwa wapinzani wao Yanga baada ya Simba kumpata MO Dewji