Jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Njombe imefanya dua maalum ya kumuombea Rais Dkt,Samia Suluhu katika msikiti wa wilaya uliopo Njombe mjini kwa lengo la kumuombea afya njema na ujasiri wa kuendelea kuliongoza taifa kutokana na shughuli kubwa alizofanya kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu tangu alipoingia madarakani.
Akizungumza mara baada ya Dua hiyo iliyoambatana na Iftar Mwenyekiti wa UVCCM Sam Mgaya amesema lengo kubwa ni kumuombea baraka na Kheri ili aendelee kutekeleza kwa ufanisi majukumu huku mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa akisisitiza watanzania kuendelea kutunza amani.
“Tumefanya hivi kutokana na kazi kubwa anayoifanya kwenye makundi yote,na ukiangalia Rais amefanya vizuri kwenye miundombinu ya afya,sekta ya elimu na maeneo mengine ndio maana tumeona kuna haja kubwa ya kumuombea”amesema Sam Mwenyekiti wa UVCCM
“Lakini wapo watu wanaopenda kuvuruga amani sisi tunaka amani ili maendeleo yaje na ukiangalia nchi yetu ni ya amani ndio maana hata mimi Kissa leo nimekuja msikitini”amesema DC Kissa
Kwa upande wake Sheikh wa wilaya ya Njombe Shaban Dinga amesema waislamu wataendelea kumuunga mkono Rais Samia kutokana na kazi kubwa anazofanya hivyo anastahili kuendelea kuiongoza Tanzania.
“Mama huyu ikiwa inampendeza allah amemuweka kwa afya njema basi anafaa kutuongoza kwa kipindi kinachofuata kwa maana ametekeleza mahitaji ya watanzania”amesema Dinga
[2:47 pm, 05/04/2024] Geena Tza: ok]