Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) akitangaza kusitishwa kwa ziara ya Kamati ya Utekeleji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa iliyokua ianze leo tarehe 11 Februari, 2024 Mkoani Arusha kutokana na Msiba wa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoya Lowassa uliotokea tarehe 10 Februari, 2024 Jijini Dar es salaam.
Aidha Ndugu Kawaida kwa niaba ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ametuma Salamu za rambirambi kwa Familia ya Hayati Edward Lowassa pamoja na Watanzania wote kwa kuondokewa na Mpendwa wao na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu.