Uwanja wa taifa wa zamani ambao kwa sasa unajulikana kama uwanja wa Uhuru au shamba la bibi, umefungwa kwa muda mrefu ili kupisha ukarabati wa uwanja huo, kwa muda mrefu uwanja wa Uhuru tumekuwa tukiona ukitumika kwa shughuli za kitaifa kama siku ya Uhuru na nyinginezo, bado mafundi wanaendelea na ukarabati.
Huenda ukawa hujabahatika kupata nafasi ya kuona maendeleo ya uwanja huo kwa hizi siku za karibuni toka ufungwe, ripota wa millardayo.com nilipata nafasi ya kukupigia picha 29 za ukarabati ulipofikia. Kwa asilimia kubwa sehemu iliyofanyiwa matengenezo ni majukwaa ya mzunguuko ambayo awali yalikuwa na vyuma, na juu hayakuwa na paa.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos