Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania – UWT inayoongozwa Mwenyekiti wake Mary Pius Chatanda imetoa shukrani na pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulipa kipaumbele suala la afya hususai mama na mtoto ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira kwa wanawake wanaojifungua watoto kabla ya wakati (watoto njiti).
Pongezi hizo zimefuatia baada ya Kauli iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Isdor Mango katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika jana tarehe 01 Mei, 2024 jijini Arusha ambapo alisisitiza kuwa likizo ya uzazi ni haki ya kila mzazi kwa kuelekeza ifuatavyo
“Iwapo mfanyakazi atajifungua moto au watoto njiti, kipindi cha uangalizi maalum hakitahesabiwa kama likizo ya uzazi. Likizo ya uzazi itaanza pale mtoto atakapomaliza kipindi cha uangalizi maalum kadri madaktari watakavyothibitisha lakini vilevile mfanyakazi husika ataruhusiwa kutoka kazini saa saba na nusu mchana kila siku kwa muda wa miezi sita baada ya kumalizika kwa likizo ya uzazi ili kumpa fursa ya kwenda kunyonyesha”Alisema Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango
Aidha UWT imetoa rai kwa serikali kuharakisha mchakato wa marekebisho ya sheria ya
Ajira na uhusiano kazini sura 366 ili itumike pia kwa upande wa wanawake wafanyakazi wa sekta binafsi nchini.
Katika taarifa yake UWT imeeleza kuwa imatambua mchango wa wadau mbalimbali ikiwemo Vyama vya Wafanyakazi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwa upekee imewapongeza Wabunge Wanawake kwa kuibeba Ajenda ya Mtoto Njiti ipasavyo na kuwa mstari wa mbele kupeleka mapendekezo hayo yaliyofanyiwa kazi na Serikali Sikivu ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.