Jumuiya ya Umoja wa wanawake nchini kupitia Chama Cha Mapinduzi (UWT) imewatoa hofu wawekezaji wote na wale wenye malengo ya kufanya uwekezaji nchini kwani Uwekezaji ni Utekelezaji wa dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuongeza pato la Taifa kupitia katika Uwekezaji sekta mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Jumuiya UWT Joketi Urban Mwegelo wakati alipokutana na wawekezaji kutoka china katika jimbo la Changzho walioletwa nchini na kampuni ya Amec Group kwa kushirikiana na Makampuni ya Wachina nchini kwa lengo la kujadiliana na kuangalia namna ya kushirikiana kwenye maeneo ya uwekezaji.
” Sisi kama UWT tupo katika mikakati ya kuwasaidia Wanawake Zaidi leo ni furaha kubwa kwetu kuwapokea wawekezaji na tumelenga zaidi katika kumuwezesha mwanamke hivyo chochote watakachoanzisha kitamgusa mwanamke moja kwa moja lengo kuwainua kiuchumi zaidi “, AmesemaMwegelo.
Hata hivyo Katibu Mkuu UWT Joketi Mwegelo Amesema “ugeni umekuja kwa wakati muafaka ambapo Chama Cha Mapinduzi CCM kimetoa maelekezo kwa jumuiya zake zote kujitegemea kiuchumi na sisi UWT tunampango wa kuzalisha mkaa mbadala unaotokana na mavumbi ya maakaa ya mawe hivyo kutokana na wawekezaji hao kujikita zaidi kwenye teknolojia itawasaidia kutumia teknolijia hiyo katika uzalishaji”.