Mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anayekipiga katika club ya Man United Alex Sanchez bado anaendelea kuwa na wakati mgumu katika kipindi hiki akiwa na Man United, Sanchez anaingia katika wakati mgumu kufuatia kupata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa mara nyingine tena.
Sanchez siku ya Jumamosi ya February 2 2019 alikuwa sehemu ya kikosi cha Man United kilichocheza dhidi ya Southampton na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 lakini alicheza game hiyo kwa dakika 52 na kutolewa kutokana na kuumia goti katika mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Dalot.
Baada ya kupata majeraha hayo inaripotiwa kuwa Alex Sanchez anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita hadi nane akiuguza jeraha hilo alilolipata katika game dhidi ya Southampton, hivyo hiyo ni kwa mujibu wa Physio wa Chile Pedro Onate kuwa Sanchez anaweza akawa nje ya uwanja kwa miezi miwili.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake