Leo July 23, 2017 issue mbalimbali zimejadiliwa kwenye Magazeti ya Tanzania ambapo moja kati ya issue hizo ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro kuwaonya Polisi wanaofanya vitendo vya dhuluma dhidi ya raia kwani vinawashushia hadhi yao.
Hiyo na nyingine nyingi nimekukusanyia kutoka kwenye twitter @millardayo na kukuwekea millardayo.com.
Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amekosoa uendeshwaji wa Bunge akisema Spika Ndugai ameshindwa kukisimamia chombo hicho. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Mkazi wa Tarafa ya Gairo, Kilosa, Rebeca Mwendi (38) amejifungua watoto walioungana kifuani hadi tumboni wakichangia kitovu. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
"Sikiliza zaidi anayekukosoa, kidogo kwa anayekusifia, wasome wote kisha fanya jambo." – Rais wa Rwanda Paul Kagame. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Inakadiriwa watu 55m watapoteza maisha kutokana na magonjwa yasiyoambukiza ifikapo 2030 kama hazitafanywa juhudi kukabiliana nayo #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amewaonya Polisi kuacha vitendo vya dhuluma dhidi ya raia kwa ni vinawashushia hadhi. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Mwanasheria Mkuu wa MSD amedai Mahakamani Bodi ilipitisha manunuzi ya pampasi 300,000 lakini uongozi uliongeza kiwango mara 2 yake. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Kaimu Kamanda wa Polisi DSM Lucas Mkondya amesema hawatomuachia Lissu mpaka watakapokamilisha upelelezi na kumfikisha Mahakamani. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Mtanzania aliyejulikana kwa jina moja la Shentel (22) anashikiliwa na Polisi India akidaiwa kukutwa na dawa za kulevya 300gm. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Mahakama ya Wilaya Maswa imemhukumu kifungo cha miaka 5 jela Sayi Mahona kwa kumiliki silaha aina ya gobole bila kibali. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 60 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Songwe kujirekebisha kabla hajamtumbua. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
BAWACHA limesema matukio ya viongozi wao wa kitaifa kukamatwa mara kwa mara hayawatishi na hawakati tamaa bali huwapa ari. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
DC wa Ukerewe Estomiah Chang'ah amesema wanajipanga kuendesha operesheni ya kuwakamata wazururaji na kuwafikisha Mahakamani. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
IGP Sirro amewataka Askari wa Jeshi hilo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria na taratibu ili kujenga taswira chanya. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
TRA Tanga imekamata bidhaa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Tsh. 40m zilizokuwa zinasafirishwa kwa boti kwa njia za panya. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Madereva wawili wa Usangu Logistics wamefariki baada ya gari la mizigo walilokuwa wanasafiri nalo kutumbukia kwenye Mto Wami. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
Watu wawili wamekufa na wengine 36 kujeruhiwa baada ya daladala kugonga kichwa cha treni, Tandika, Dar es Salaam. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 23, 2017
ULIKOSA? Wizara Mambo ya Ndani, IGP Sirro wazungumza kuhusu mauaji Kibiti…bonyeza play hapa chini kutazama!!!