Leo December 4, 2017 katika kongamano la wataalamu wa ununuzi na ugavi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dr Philip Mpango amesema kuwa katika kutekeleza shughuli za ununuzi na ugavi nchini miradi saba iliyokaguliwa nchini yenye thamani ya Tsh Bilion 2 imetekelezwa katika kiwango zisichoridhishwa.
Ameeleza pia kuwa kwa upande wa maadili ,ukaguzi umebaini kuwepo kwa viashirio vingi vya rushwa katika usimamizi wa miradi 33 katika taasisi 17 za umma. Katika ukaguzi huo wa taasisi tatu ilibainika kiasi cha Tsh Milioni 488.9 zililipwa kwa wakandarasi bila kuwepo kwa kazi yoyote iliyofanyika.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Samia Suluhu ameiagiza bodi ya ununuzi na ugavi nchini PSPTB kuchukua hatua kali kwa taasisi za umma na binafsi zinazoendelea kuajiri watumishi wa ununuzi na ugavi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo.
Ametoa onyo pia kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaoendekeza vitendo viovu kama rushwa ,upendeleo,wizi na uzembe waache mara moja kwani hatua kali zitachukuliwa kwa yoyote atakayekwenda kinyume na maadili ya kazi yao.
Ulipitwa na hii? Agizo la Kigwangalla baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini